Kuna fununu ambazo zimejaa midomoni kuhusu umiliki wa gari kali ya msanii mwenye sauti kali mmiliki wa Bendi ya Malaika maarufu kama King of the Best Melody, Christian Bella anaetamba na ngoma ambayo ameshirikiana na Alikiba inayojulikana kama Nagharamia, iliyofanya chini ya umahiri mkubwa wa mtayarishaji Abydad.
Christian Bella amefunguka na kueleza uvumi huo na kuweka wazi kuwa hakuna mtu yeyote anaemsaidia katika shughuli zake za muziki na gari analomiliki amenunua kwa pesa zake mwenyewe, ambazo amezipata kutokana na show anazozifanya.
Post a Comment