NAIROBI,Kenya.
KIONGOZI wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis mara baada ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jana na kuelekea Ikulu kuungana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta moja ya kazi kubwa aliyoifanya ni pamoja na kupanda mti wa ukumbusho.
Papa Francis ambaye aliambatana na msafara wa watu wake kutoka Vatican na ujumbe wa kanisa katoliki nchini Kenya,alifanya tukio hilo katika Ikulu ya Kenya huku akishuhudiwa na Rais Kenyatta na makamu wake Wiliamu Rutho.
Post a Comment