SAKATA LA DIAMOND KUTOBOA PUA HILI HAPA


Kwa saa kadhaa zimeenea taarifa za mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kuonekana katoboa pua, hii habari imepewa nguvu kutokana na picha aliyoipost Diamond mwenyewe kwenye Instagram akionekana katoboa pua.
Ukweli ukoje? …ukweli ni kwamba Diamond hajatoboa pua kama wengi walivyodhani ambapo Meneja wake aitwae Sallam aliwajibu hivi mashabiki walioanza kuuliza >>> ‘Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo’
SK
Maneno ya Meneja Sallam yanamaanisha kwamba sio kweli Diamond katoboa pua, ni mchezo tu na baada ya hiyo picha ya kutoboa pua Diamond aliweka picha nyingine inayoonekana hapa chini akiwa fresh kabisa watu wasiendelee kupanic.
Diamond 2

TAZAMA PICHA ZA ZAMANI ZA MASTAA WA BONGO


Ni TBT!! Throwing back thursday ambapo huwa tunaitumia hii siku kushare zile picha zetu za zamani ambapo kwenye millardayo.com kila wiki tutakua tunakuletea picha mbalimbali za mastaa wakiwa kwenye pozi miaka kadhaa iliyopita.
.
.Producer Hermy B kwenye udogo wake
.
.Rapper Izzo Bizness kwenye udogo wake
.
.Msanii wa Bongo Fleva, Linex enzi hizo
.
.Kushoto ni Msanii wa RNB, Ben Pol enzi hizo
.
.Ray C enzi hizo #TBT
.
.Kushoto ni Nikki wa pili enzi hizo akiwa shuleni
.
.Rais Magufuli enzi hizo
.
.Kulia ni msanii wa Bongo Movies, Rose Ndauka enzi hizo

HIZI NDIZO VIDEO 25 ZA BONGO FLEVA ZILIZOTAZAMWA ZAIDI

Kukua kwa teknolojia kumeufanya muziki usambae kwa haraka zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Kwa sasa watu wengi huzitazama video za muziki kwenye simu zao zaidi kuliko hata kwenye TV zao.
youtube-logo-name-1920
Infact huanza kuziona video mpya kwenye smartphones zao dakika chache tu baada ya video kuwekwa Youtube.
Mwaka huu zimetoka video nyingi nzuri za muziki lakini si zote zilizopata views nyingi. Tumeangalia video 25 zilizotazamwa zaidi kwa mwaka 2015.
Video hizi ni zile zilizotoka kuanzia January hadi December, 2015.
Utagundua kuwa kuna baadhi ya video zina muda mfupi tu lakini zina views nyingi. Hii ina maana kuwa baada ya wiki au miezi michache zinaweza kupanda nafasi za juu zaidi na chati hii ikabadilika. Kwa sasa hizi ndiyo video za Bongo Flava zilizotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube.
1. NANA – DIAMOND PLATNUMZ F/ FLAVOUR
Views milioni 7.9 ndani ya miezi sita
2. NASEMA NAWE – DIAMOND PLATNUMZ F/ KHADIJA KOPA
Views milioni 5.9 ndani ya miezi minane
3. NITAKUPWELEPWETA – YAMOTO BAND
Views milioni 2.6 ndani ya miezi 11
4. CHEKECHA CHEKETUA – ALIKIBA
Views 2,045,412 ndani ya miezi mitano
5. NISAMBAZIE RAHA – YAMOTO BAND
Views 1,508,229 ndani ya miezi sita
6.NA YULE – RUBY
Views 1,142,726 ndani ya miezi saba
7. SALIMA – LINEX F/ DIAMOND
Views 1,138,258 ndani ya miezi tisa
8. UTANIPENDA – DIAMOND PLATNUMZ
Views milioni 1.1 (video yenye subtitle za Kiingereza)
Views 984,276 (video isiyo na subtitle)
Ndani ya wiki mbili
9. CHEZA KWA MADOIDO – YAMOTO BAND
Views milioni 1.18 ndani ya miezi mitatu
10. NOBODY BUT ME – VANESSA MDEE
Views 946,785 ndani ya miezi tisa
11. WANJERA – OMMY DIMPOZ
Views 879,104 ndani ya miezi tisa
12. NASHINDWA – CHRISTIAN BELLA
Views 720,893 ndani ya miezi minane
13. NIKUITE NANI – JUX
Views 626,335 ndani ya miezi tisa
14. GAME – NAVY KENZO F/ VANESSA MDEE
Views 579,820 ndani ya miezi mitano
15. SHIKOROBO – SHETTA F/ KCEE
Views 563,559 ndani ya miezi tisa
16. SIRI – VANESSA MDEE & BARNABA
Views 546,083 ndani ya miezi kumi
17. LOOKING FOR YOU – JUX F/ JOH MAKINI
503,523 ndani ya miezi minne
18. AIYOLA – HARMONIZE
Views 484,932 ndani ya miezi miwili
19. NITAZOEA – MO MUSIC
Views 451,863 ndani ya miezi saba
20. SOPHIA – BEN POL
Views 444,569 ndani ya miezi minane
21. HELLO – LINAH F/ CHRISTIAN BELLA
Views 408,454 ndani ya miezi minane
22. NUSU NUSU – JOH MAKINI
Views 405,610 ndani ya miezi minane
23.NEVER EVER – VANESSA MDEE
Views 401,556 ndani ya miezi miwili
24. KAUNYAKA – CHEGE & TEMBA
384,929 views ndani ya kumi
25. DON’T BOTHER – JOH MAKINI F/ AKA
Views 349,967 ndani ya miezi miwili
Bonus
NAGHARAMIA – ALIKIBA & CHRISTIAN BELLA
342,218 views ndani ya wiki moja
HAPO ULIPO – MIRROR
Views 222,521 ndani ya miezi minne


DIAMOND PLATNUMZ AFUNIKA ONESHO LA DAR LIVE


IMG_7177Mwanamuziki mahiri wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akifanya yake katika onesho lakendani ya  Dar Live.
IMG_7181IMG_7194IMG_7212IMG_7228IMG_7242IMG_7260IMG_7262IMG_7269IMG_7270IMG_7287

WAIGIZAJI HAWA WACHUANA VIKALI KUIGIZA FILAMU YA OBAMA


obamaMwigizaji kutoka Marekani Will Smith ameweka wazi kuwa ana wasi wasi staa wa filamu wa Uingereza Idris Elba anawza kuimba ndoto yake ya kuigiza kama Obama kwenye filamu ya maisha ya rais huyu. Filamu hii inayomzungumzia rais wa 44 inategemewa kuwa kubwa na kugusa wengi.
Will Smith aliulizwa kuhusu kuigiza kama Obama akasema “Wiki chache zilizopita mimi na Obama tuliongea jambo hilo“.
Na kuhusu Idris Elba kuiba nafasi hio ya kuigiza kama Obama Will Smith amesema “Idris ana lafudhi ya Uingereza na akiongea anasikika kama msomii sanaa, mimi nimesha fanya mazoezi ya kuongea kama Obama, sasa yeye ajipange“.
alg-smith-elba-jpg

50 CENT AMSHTAKI RICK ROSS KWA KUTUMIA BEAT YA IN DA CLUB KWENYE MIXTAPE YAKE


50 na rozay
Rapa 50 Cent afungua kesi dhidi ya rapa Rick Ross akidai katumia mdundo wake wa In Da Club kwenye mixtape yake bila ruhusa yake.
50 Cent anadai fidia ya dola milioni mbili kutoka kwa Rick Ross kama fidia ya kutumia mdundo wa “In Da Club,” kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.
Wimbo huu upo kwenye mixtape ya Rick Ross ya Renzel Remixes project na 50 Cent amesema Rozay amefnya wimbo huo na kazi hio ilikupata pesa za kutangaza album yake mpya ya Black Market.

KALI YA MWAKA | WAUMINI KANISANI WASHEREHEKEA FILAMU HII

Watoto walivalia mavazi ya Darth Vader kama ishara ya kusherehekea kwa kutolewa kwa filamu mpya ya Star wars katika kanisa moja jijini Berlin siku ya Jumapili

Waumini katika kanisa la Zion Church walianza ibada yao kwa kuonyesha mfululizo wa matukio kwa ufupi ya filamu hiyo ya Star Wars huku kasisi akiendeleza ibada hiyo kwa mafunzo kutoka kwa filamu hiyo.


Kasisi huyo akihutubia takriban waumini 500 alisema kuwa filamu hiyo ya Star Wars ina mafunzo ya kuhusu  kushinda ubaya kwa wema ambayo pia inapatikana katika Agano jipya la biblia ya kikristo.

Wakati huo huo baadhi ya vyombo vya habari vya kijamii vilikashifu kitendo hicho kanisani wakikosoa kwa kusemani kitendo cha dhambi na fedheha.

Lakini kasisi Eva-Maria Menard alisisitiza kuwa kushughulikia masuala ya kisasa na dini ni njia pia ya kuelimisha jamii zaidi.

IDADI YA WALIOTAZAMA VIDEO YA ALI KIBA YAZUA MASWALI



Video ya Nagharamia ina siku tatu tangu itoke na kutimiza watazamaji 95,723 huku nyimbo ya Utaipenda ya Diamond kipindi inatoka ilitimiza watazamaji lakitatu ndani ya siku tatu, kitu kilichopelekea mashabiki hao kusema kuwa Alikiba haungwi mkono na mastaa wenzake pindi anapotoa kazi zake tofauti wanavyofanya wengine,



HIZI NDIZO MUVI KALI ZA BONGO ZILIZOINGIA KWENYE TUZO ZA AMVCA 2016


Ni kitu kizuri sana kukuta sanaa ya Tanzania inatoboa na kugusa headlines nje ya mipaka ya Tanzania, kama vile ambavyo tumeona Tuzo kadhaa za muziki zikiletwa TZ na mastaa wetu kutoka nje ya mipaka, basi nikusogezee na hii list ya mastaa ambao wamefanikiwa kuwa sehemu ya walioingia kwenye category za Africa Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCAs).
Kwenye list ya Watanzania wako na hawa:
1: Staford Kihore (Movie ya Mpango Mbaya)
2: Josephat Lukaza (Movie ya Kitendawili)
3: Elizabeth Michael ‘Lulu’ (Movie ya Mapenzi ya MUNGU)
4: Amil Shivji (Movie ya Samaki Mchangani)
TUZO
List ya washiriki wote hii hapa mtu wangu, na Watanzania wetu wote ndani.
NOMINEES II NOMINEES III NOMINEES IV NOMINEES IX NOMINEES V NOMINEES VI NOMINEES VII NOMINEES VIII NOMINEES X NOMINEES XI NOMINEES XII NOMINEES XIII NOMINEES XIV NOMINEES XV
Unaweza kuingia kwenye link hii kwa ajili ya kupiga kura >>> amvca201
6

OUJUELEGBA NDIO WIMBO NAMBA 12 BORA ZAIDI DUNIANI


IMG_5365
Wimbo wa WizKid ‘Ojuelegba Remix’ watajwa kuwa No 12 kwneye nyimbo bora za 2015 na jarida la Fader kwenye orodha ya nyimbo 107 bora za mwaka 2015.
Wimbo huu wa ‘Ojuelegba Remix’ unasauti ya rapa Drake kutoka Marekani na  Skepta kutoka Uingereza.
Jarida la Fader limeandika haya kuhusu wimbo huu.
“Drake ameingia kwenye wimbo wa huyu msanii kutoka Nigeria na kuupa umaarufu zaidi Marekani, vesi ya Drake na Skepta zimeipendezesha zaidi “Ojuelegba” lakini ukweli ni kuwa wimbo huu tayari ulikuwa mkubwa sana Marekani na nchi zingine, wimbo unaujumbe mzuri wa shukurani na matumaini kuhusu nyumbani kwao”.
Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top