JINA la Rais Magufuli limeendelea kubeba vichwa vya habari vya redio ,luninga na magazeti mengi ya Afrika mashariki kutokana na jinsi ya maamuzi yake magumu yanavyohatarisha ulaji wa ‘waliokuwa’ wajanja wachache waliokuwa wanaiibia Serikali kimyakimya.
Nchini Kenya moja ya gazeti kubwa la habari za baishara limeandika juu ya mkakati huo wa Magufuli kutishia uhai wa kiwanda cha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa maziwa kinachoitwa Brookeside Ltd ambacho kimekuwa kikiwanyonya wananchi wa Arusha kwa kununua maziwa kwa bei chee na kwenda kuyauzia Kenya
Post a Comment