Serikali Yakanusha Madai Kuwa Haina Mpango wa Kuwapanga Vijana Waliohitimu Kidato cha Nne kwenda kidato cha Tano


Serikali imekanusha madai ya  kuwepo kwa taarifa ya kuwa haina mpango wa kuwapanga vijana waliohitimu kidato cha nne kwenda kidato cha tano kwa sababu mbalimbali.

Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa taarifa hizo ni za uvumi na serikali kwa sasa ipo katika mchakato wa upangaji wa majina hayo na wakati wowote mwisho mwa mwezi majina yatakuwa yametolewa.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema moja ya sababu za kuchelewa kwa matokeo hayo ni pamoja na wizara kubadili mfumo wa GPA, kwenda Division hivyo mchakato huo ndio unafanywa na serikali ili wanafunzi wote wapate madaraja yao na waweze kupangiwa shule.

Mhe. Majaliwa amesema suala la upangaji halikuwa kwa kidato cha tano peke yake bali pia wale wanaokwenda vyuo mbalimbali na kusema kuwa baada ya kukamilika watatoa majibu yao wiki mbili kabla ili wazazi waweze kujiandaa kuwapeleka watoto mashuleni.

Magufuli: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Pumzika Kwa Amani.......Wewe upo Salama, Usisikilize kelele za Nje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kwamba serikali itawalinda wastaafu nchini wakiongozwa na viongozi wakuu wa umma ili wawe na heshma yao ndani ya jamii.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa tume ya taifa ya uchaguzi.

''Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wewe pumzika kwa raha zako , upo salama watachonga wee lakini mimi kama Rais wa awamu ya tano nipo tayari kuwalinda watumishi wote wastaafu kwa kuthamini mchango wao ndani ya taifa hili''

Aidha Rais Magufuli amesisitiza kwamba uchaguzi nchini umemalizika hivyo vyama vyote vya siasa viongeze nguvu baada ya miaka mitano ili apimwe na wananchi waliomchagua kama ametekeleza ahadi zake.

''Niwaombe wanasiasa wenzangu uchaguzi umekwisha, kama ni wabunge jielekezeni bungeni, kama ni madiwani jielekezeni kwenye maeneo yenu, sitakubali mtu yeyote anikwamishe katika kutimiza ahadi zangu kwa wananchi'' Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu tume ya uchaguzi kukabiliwa na changamoto lukuki Rais Dkt. Magufuli amesema fedha za tume hiyo ilizobakiza kiasi cha shilingi bilioni 12 na kuzirudisha serikalini, serikali imeruhusu fedha hizo zitumike kujenga jengo la tume hiyo ili kuondokana na gharama za kupangisha jengo wanalotumia kwa sasa.

Aidha akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva amesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa huru na wa haki na hata waangalizi wa nje wengi wamepongeza uchaguzi huo.

VIONGOZI WA CUF WAPONDWA KWA KUKOSA UZALENDO.


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekishiutumu Chama cha Wananchi (Cuf) pamoja na viongozi wao kwa kukosa uzalendo kutokana na kauli zao za kuunga mkono wahisani kuisitishia misaada Tanzania.

Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa kuteuliwa kutoka katika chama cha Ada-Tadea, Juma Ali Khatib ambaye aligombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa marudio, alipokuwa akichangia hotuba ya Rais wa Zanzibar kwenye baraza hilo mjini hapa.

Alisema, viongozi wa Cuf wameonesha udhaifu mkubwa wa kukosa uzalendo kwa kitendo chao cha kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa misaada kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema, Zanzibar ni nchi yenye kufuata katiba yake kwa hiyo ilikuwa na mamlaka kamili kupitia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kuitisha uchaguzi wa marudio baada ya kuufuta wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Nimesikitishwa na kauli za viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kuhusu uamuzi wa kususia misaada kwa Tanzania. Viongozi hao wameonesha udhaifu na kukosa uzalendo,”alisema Khatib.

Alisema chama chake kiliamua kuingia katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kwa sababu umeitishwa na chombo halali kwa mujibu wa katiba, chenye majukumu ya kusimamia uchaguzi kikiwa hakiingiliwi na mtu yeyote.

Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini , Machano Othman Said, alisema kitendo cha viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa kutoa misaada kwa Tanzania hakikubaliki hata kidogo kikionesha udhaifu mkubwa wa viongozi hao katika uzalendo wa nchi.

KILICHOJIRI KESI YA PINGAMIZI LA STEPHEN WASIRA DHIDI YA ESTER BULAYA MAHAKAMANI

Mahakamaa Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali maombi ya baadhi ya wapigakura wa Jimbo la Bunda Mjini ya kuruhusiwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Makahama Kuu wa kufuta shauri lao la kupinga matokeo ya uchaguzi.

Maombi hayo yaliwasilishwa na Magambo Masato na wenzake wanne wanaompigania Stephen Wassira, wakiiomba mahakama hiyo kuwaruhusu kukata rufaa Mahakama ya Rufani baada ya kutoridhiswa na uamuzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema), dhidi ya Stephen Wasira (CCM).

Jaji anayesikiliza shauri hilo namba 25 la mwaka 2016, Rose Ebrahim alisema jana kuwa anakubaliana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi kuwa hayana mashiko kisheria.

Pingamizi hilo lilowasilishwa na Wakili Mfawidhi wa Serikali, Paschael Marungu alidai aliyesaini hati ya maombi siyo aliyethibitisha kwani hilo ni kosa la kisheria.

Wakili Marungu alidai hati hiyo ilisaniwa na Wakili Denis Kahangwa na kuthibitishwa na Wakili Constantine Mutalemwa kwamba hilo ni kosa kisheria, hivyo kuiomba mahakama kutupilia mbali.

Akitoa uamuzi juu ya pingamizi hilo, Jaji Ebrahim alisema anakubaliana na pingamizi hilo kwani, makosa yaliyofanywa hayarekebishiki.

“Haya maombi nayatupilia mbali hayana miguu ya kusimamia, ni kosa kubwa hati kusainiwa na mtu mwingine halafu ikathibitishwa na mwingine, hakuna namna ya kurekebisha, lazima sheria ifuatwe na taratibu zake,” alisema.

Awali, Magambo na wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga ushindi wa Bulaya, lakini ilitupiliwa mbali kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya sheria.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, Bulaya alipata kura 29,973 na Wasira wa CCM aliambulia 19,123 ikiwapo tofauti ya kura 10,000.

Hata hivyo, Wasira alilalamikia matokeo hayo akidai uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu.

HIZI NDIZO ADHABU ZA WANAOKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Wenzetu China hawana mzaha kwa wanaokamatwa wakisafirisha dawa za kulevya 'punda'. Wao sheria zao zinaruhusu hata kupigwa shaba kama hivi...



 ...tena mbele ya halaiki ya watu ili iwe fundisho kwa watu wote wajue jinsi walivyo makini na ishu hizo.

WAZIRI SIMBA CHAWENE APONGEZA KIMAMISHWA KWA UCHAGUZI WA MEYA DAR


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imetumia busara kuahirisha uchaguzi wa Meya uliopangwa kufanyika leo.

Juzi halmashauri hiyo, iliahirisha uchaguzi huo, ikiwa ni mara ya pili baada ya kubaini nyongeza ya wajumbe 14 katika orodha iliyowasilishwa kwa wakurugenzi wa Manispaa za Kinondoni na Ilala.

Kasoro hizo zilijitokeza katika kikao cha viongozi wa halmashauri hiyo kilichongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Sarah Yohana na kuhudhuriwa na viongozi wa CCM, Chadema na CUF kujadili ajenda mbili.

Ajenda hizo ni taratibu za kuendesha uchaguzi wa Meya na kupitia orodha ya wajumbe wanaostahili kushiriki.

Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Yohana kuwaagiza wakurugenzi wa manispaa za Kinondoni na Ilala kuyafanyia uhakiki majina hayo wakishirikiana na viongozi wa vyama ili kuyapeleka halmashauri kesho kutwa.

Simbachawene alisema jana kuwa halmashauri na viongozi wa vyama hivyo walitafakari maelezo aliyoyatoa awali kabla kufikia hatua ya uchaguzi huo.

“Sijapata taarifa za kuahirishwa ndiyo kwanza nasikia kwako, lakini kama sababu ndiyo uliyoniambia basi wamefanya jambo jema. Kwa sababu uchaguzi huu una mvutano hivyo ni lazima mambo yaende kwa makubaliano.

“Pia ni hatua nzuri, itakayoleta maelewano baina yao ili kupata haki sawa kwa wajumbe watakaostahili kupiga kura. Tamisemi kazi yetu ni kueleza sheria inasemaje,” Simbachawene.

Hivi karibuni, Simbachawene aliahirisha uchaguzi huo, kisha kutoa sababu kuwa ni kuandaa mfumo wa upatikanaji wa wajumbe kutoka manispaa tatu kwa kuwa ule wa chama kimoja haukuwa na shida kama ilivyo sasa.

Katibu wa Chadema, Kanda ya Dar es Salaam, Henry Kilewo alisema kukwama kwa uchaguzi huo kunatokana na viongozi kutosikiliza mawazo ya upinzani.

 “Januari 27, nilimwandikia barua Simbachawene ya kutaka atupatie utaratibu wa uchaguzi huu utakavyokuwa, lakini hadi leo (jana), hakunijibu ndiyo maana matatizo kama haya yanatokea,” alisema.

MAWAZIRI MRAMBA NA YONA WAKABIDHIWA VIFAA VYA USAFI WAKIELEKEA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE


Mawaziri wa zamani Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona wameripoti leo katika hospitali ya Sinza Palestina na kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kufanya usafi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliridhia Mawaziri hawa  wastaafu kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.

MWENYEKITI WA KIJIJI WA CHADEMA AKATALIWA



Wakazi wa Kitongoji cha Misungwi D, Kijiji cha Misungwi wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza wamemkataa Mwenyekiti wao, Raphael Kimoka (Chadema) kwa tuhuma za kutowasomea taarifa za mapato na matumizi ya fedha tangu achaguliwe.

Walitoa msimamo huo kwenye mkutano mkuu wa kitongoji uliofanyika juzi.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Misungwi, Amos Seko alisema wakazi hao wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli za maendeleo, huku wakiendelea na vikao na kuweka maazimio ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wao.

“Leo ni kikao cha mwisho kuhusiana na malalamiko yenu dhidi ya mwenyekiti mliyoyaleta tangu Oktoba 27, mwaka jana. Mtaamua wenyewe hapa ama aendelee au la,” alisema Seko.

Seko alisoma tuhuma nyingine dhidi ya mwenyekiti zilizopelekwa kwake na wakazi hao kuwa ni kutosimamia majukumu yake vizuri, kubagua wananchi wakati wa kutoa huduma, kutohudhuria vikao vya kitongoji vya maafa na kutetea uhalifu.

Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ambaye ni Ofisa Tarafa wa Misungwi, Peter Marco alisema tuhuma dhidi ya mwenyekiti huyo ziliwasilishwa kwenye kikao cha halmashauri ya kijiji cha Novemba 11, mwaka jana, Alisema kiongozi huyo alipewa nafasi ya kujitetea, lakini hakufanya hivyo badala yake alitoka nje ya kikao.

Kimoka alipopewa nafasi ya kujitetea, alidai kuwa mkutano huo umeandaliwa kisiasa, hivyo hautambui kwa sababu wengi wao ni wanachama wa CCM.

“Waliohudhuria hawakunitendea haki, sikubaliani nao,” alisema.

Aliongeza kuwa, kwa muda mrefu alijua kulikuwa na mpango wa kutaka kumuondoa madarakani wenye msukumo wa kisiasa.

LOWASA AUNGA MKONO CUF KUJITOA KATIKA MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR

Ni dhahiri kuwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema bado ana ndoto za kuwa rais wa Tanzania baada ya kurudia kauli yake ya kwenda Ikulu, lakini safari hii akisema chama hicho kitaingia Ikulu bila ya kumwaga damu.

Lowasa alisema hayo jana katika mkutano ulioandaliwa na Baraza la Wazee wa Chadema, tawi la Ubungo kwa ajili ya kumpongeza kwa ushupavu aliounyesha baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

“Siku moja tutaingia Ikulu bila kumwaga damu. Msiwe na wasiwasi kwa sababu mimi, dunia na Watanzania wanafahamu kuwa tulishinda katika uchaguzi uliopita,” alisema Lowassa ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu.

Lowasa alisema ingawa ana uhakika kuwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita yalichakachuliwa, aliweka mbele amani.

“Nawashukuru Watanzania kwa kunisikiliza, walikuwa wananisikiliza mimi tu baada ya uchaguzi. Ningeweza kuwaambia twende barabarani, sikufanya hivyo kwa sababu najua amani ni muhimu,” alisema.

Uchaguzi wa Zanzibar 
Waziri huyo mkuu wa zamani pia alizungumzia uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi wa rais, wawakilishi na madiwani Machi 20, akitahadharisha kuwa suala hilo linaweza kusababisha mpasuko.

“Hali ya Zanzibar isiposhughulikiwa kwa umakini na umahiri, italeta matatizo makubwa nchini,” alisema.

Alimtaka Rais John Magufuli, akiwa kiongozi wa Tanzania, kuchukua uamuzi na kuhakikisha suala la Zanzibar linatatuliwa.

Alisema UKAWA  inaunga mkono maamuzi ya  CUF kupinga uchaguzi huo kurudiwa kwa kuwa hakuna ushahidi wa kukiukwa kwa taratibu zozote za uchaguzi wa mwaka jana.

“Nashauri wakae chini wazungumze, kwa nini hili la sasa linashindikana wakati CUF walikubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa miaka mitano?” alihoji.

Alisema amani ni jambo la muhimu na linatakiwa lipewe kipaumbele kabla ya uamuzi mwingine kufanyika.

Kuhusu mikakati ya kukiboresha chama, Lowassa, ambaye alipata kura milioni 6.07 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli aliyepata kura milioni 8.8, alisisitiza uamuzi wake wa kufanya ziara nchi nzima kuwashukuru Watanzania wote ambao walimpigia kura na ambao hawakumpigia.

Lowassa pia alizungumzia uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akiituhumu kuwa inaendeshwa na chama tawala.

Alisema katika uchaguzi uliopita, NEC ilipotosha matokeo na kuharibu mchakato wa uchaguzi.

“NEC ilifanya mambo ya hovyo, walipaswa kufukuzwa, ni uongo kusema kuwa ipo huru,” alisema.

Awali, kabla ya Lowassa kusema hayo, mwenyekiti wa wazee hao wa Chadema, Enock Ngombale alisoma risala ambayo ilimpongeza kwa ushupavu aliounyesha kabla na baada ya uchaguzi.

Katika risala hiyo, Ngombale alisema Watanzania wanajua kuwa Lowasa alishinda uchaguzi, lakini walishangazwa na matokeo.

“Wewe ni kiongozi imara, shupavu na mahiri. Watanzania waliamini kuwa ulishinda lakini kilichofanyika ni uchakachuzi,” alidai.

Kadhalika, risala hiyo ilisema Serikali ya Rais Magufuli haifuati sheria na kanuni za utawala bora.

“Tumeona unyanyasaji mkubwa kwa wafanyabiashara, bomobomoa ambayo haifuati misingi ya haki za binadamu,” alisema.

Pia, wazee hao walimshauri Lowassa mambo mbalimbali ya kukiimarisha chama. 

SERIKALI YALAANI KITENDO CHA UDHALILISHWAJI ALIOFANYIWA BINTI WA KITANZANIA NCHINI INDIA


Serikali ya Tanzania imesikitishwa na inalaani vikali kitendo cha udhalilishwaji alichofanyiwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania na Kundi la watu katika jimbo la Bangalore nchini India.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi alipokutana na Wandishi wa Habari kwa ajili ya kuwaeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kitendo hicho cha kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa Kitanzania nchini India.
Balozi Mwinyi alisema kuwa, hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini India kuiandikia Serikali ya nchi hiyo kuomba maelezo kamili kuhusu tukio hilo pamoja na kuitaka Serikali ya India kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika pamoja na kuimarisha usalama katika maeneo wanayoishi wanafunzi wa Kitanzania. 
Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa amemwita Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya na kumweleza masikitiko ya Serikali ya Tanzania kufuatia kitendo hicho cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania.
Katika mazungumzo yao, Balozi Arya alieleza bayana kuwa Serikali ya India imesikitishwa na tukio hilo la udhalilishaji na kwamba Serikali imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kutekeleza uovu huo.
Alisema kuwa Waziri Mkuu wa Jimbo la Bangalore aliongea na umma kuelezea masikitiko yake kuhusu uovu huo na kuahidi kuwa mamlaka za jimbo hilo zitaimarisha usalama katika maeneo yote wanayoishi wanafunzi wa Tanzania na raia wengine kutoka nje.
Balozi Arya aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa India inaheshimu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, hivyo itashughulikia suala hilo kwa ukamilifu na hadi wakati huu tayari watu watano wanashikiliwa na vyombo vya usalama wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Sanjari na taarifa hiyo, Balozi Mwinyi aliwaomba Watanzania kutohusisha tukio hili la uhalifu na ajali ya Mtanzania, Bw. Christian Benjamin Mlyansi iliyotokea nchini India jana usiku na kusababisha kifo chake.

Alisema kuwa Bw. Mlyansi alipata ajali ya kawaida alipokuwa anaendesha pikipiki ambapo ilipoteza mwelekeo na kugonga ukingo wa kati wa barabara.

MAALIM SEIF ASISITIZA KUTOSHIRIKI MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR


Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Wazanzibari na wapenda amani kuondoa shaka na kwamba, atatangazwa kuongoza visiwa hivyo.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo kwenye viwanja vya Nngoma Hazingwa, Chake Chake Pemba akiwa na viongozi wa wilaya, majimbo na jumuiya za chama hicho ikiwa ni siku moja baada ya kufanya mkutano wa namna hiyo Unguja.

Kiongozi huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF amesema kuwa, ukweli umedhihiri ndani na nje ya nchi na kwamba hakuna sababu ya kutotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.

Amesema, “Jumuiya na waangalizi wote wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa wameshuhudia uchaguzi huo na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru, haki na wa uwazi na wanaendelea kushikilia msimamo wao kutaka mshindi wa uchaguzi huo atangazwe.”

Amesisitiza kuwa CUF haitoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu kauli ambayo pia imeungwa mkono na wafuasi wa chama hicho Pemba kama ilivyokuwa Unguja.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amemtaja Maalim Seif kuwa kiongozi aliyebobea kisiasa na anayejali maslahi ya Wazanzibari.

Katika hatua nyingine mawakilishi na madiwani wateule wa CUF  wamepanga kwenda mahakamani kutetea nafasi zao.

Wameeleza kwamba, kwa kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewapa hati za ushindi baada ya kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015, mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kupinga ushindi wao.

Hata hivyo, Maalim Seif amesema, viongozi hao waliochaguliwa na wananchi katika uchaguzi huo na kisha kupewa shahada zao, watakwenda mahakamani kutetea nafasi zao na kutoruhusu viongozi wengine wa ngazi hizo kuchaguliwa tena kwa vile wao wanavyo vielelezo vyote vya kuchaguliwa kwao.



Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura na kuthibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo, majimbo yote 18 ya uchaguzi Kisiwani Pemba yalichukuliwa na CUF, sambamba na wadi zote 32 za uchaguzi.

RAISI MAGUFULI AMUONGEZEA MUDA MWAMUNYANGE


RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo .
 
Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi.

Sanajari na huyo,Jeneral Mwanunyange amesema pia Rais Magufuli  amefanya uteuzi mkubwa ndani ya Jeshi hilo  kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya jeshi hilo.
 
Jenerali Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais  ni Meja Jenerali James Aliois Mwakibolwa  kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu ambaye amechukua nafasi ya meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu anayestaaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria ambapo Meja Mwakibolwa alikuwa ni mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu ya jeshi.

Jeneral Mwamunyange alimtaja pia  kamanda mwingine aliyeteuliwa na Rais ni Meja Jenerali Yakub Sirakwi kuwa  Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii. Meja Jenerali Sirakwi alikuwa mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.

Mwingine  aliyeteuliwa  na Rais Magufuli ni Brigedia Jenerali George William Ingram kuwa  Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga ambaye anachukua nafasi ya  Meja Jenerali Joseph  Pwani aliyestaafu leo kisheria  baada ya kufikisha umri wa kustaafu. Bregedua Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika mako makuu ya kamandi ya Jeshi la Anga.

Pia Rais Magufuli amemteua Bregedia Jeneralio M.W Isamuhyo kuwa  Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo,baada ya kufikisha umri wa kustaafu kazi kisheria,kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa mkurugenzi makao mkuu ya jeshi.

Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Jacob Kingu kuwa   mkuu wa shirika la mizinga  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Charles Muzanila anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umri .Brigedia Jeneral Kingu alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.

Pia Rais Magufuli  amemteua Bregedia Jenerali Robison Mwanjelakuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS) kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria .Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
 
Aidha,Rais Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongolekuwa   Kamanda wa Brigedia ya Tembo  kuchukua nafasi ya Brigedia Jeneral J.M Chacha ambaye anastaafu leo  kisheria baada ya kufikisha umri wa kustaafu,.Bregedia Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa Afisa Mnadhimu makao makuu ya Jeshii.
 
Rais Magufulia pia amemteua  Bregedia Jenerali Sylevesta M.Minjakuwa mkuu wa chuo cha ukamanda  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ambaye anastaafu kazi  leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria ambapo kabla ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa mkuu wa utawala katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC.

MAJANGILI YATUNGUA HELIKOPTA NA KUMUUWA RUBANI


Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.

Kufuatia tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa na kwa uhifadhi wa taifa la Tanzania.

Waziri Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo ilipotunguliwa na kuikuta helkopita hiyo iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia wa Uingereza ambae alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.

Nae kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa na kwamba watu watatu wanashikiliwa na polisi wakihojiwa kufuatia tukio hilo.

==> Hili ni tukio la kwanza  katika historia ya uhifadhi nchini mwetu kwa Majangili kumpiga  risasi na kumuua Rubani na kisha  kuangusha helikopta .

==>Kepten Roger alikuwa akienda kuongeza nguvu ya askari wa uhifadhi waliokuwa wakipambana na majangili hatari wilayani Meatu, Simiyu katika ranchi ya wanyamapori ya Mwiba.

Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top