
Kupanda kilele cha Mlima Kilimanjaro
Nyirenda ni mtu pekee ambaye kamwe hawezi kuachwa katika historia ya aina yoyote juu ya uhuru wa Tanganyika.
Ni yeye aliyepandisha mwenge wa uhuru na bendera katika mlima mrefu kuliko yote Afrika, wa Kilimanjaro Desemba 9, 1961.
Nyirenda alifanya kazi hiyo kwa ujasiri mkubwa, ikikumbukwa kuwa wakati huo, kupanda mlima huo ilikuwa ni jambo kubwa, zito na la hatari kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na barafu nyingi na watu wengi waliogopa wakiamini kuwa uwezekano wa kurudi chini ukiwa hai ulikuwa mdogo.
Akielezea tukio hilo, Nyirenda alisema msafara wa kupanda Mlima Kilimanjaro ulikuwa na watu 11, wakiwemo wapiga picha na watangazaji wa redio.
Safari yao ilianza jijini Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro ambapo walitumia jumla ya siku 16 kutimiza wajibu huo mzito.
Anasema kabla ya kuanza kupanda, walifanya mazoezi ya kupanda mlima na maandalizi mengine, kwa siku nyingi na siku hiyo walianza kupanda saa 12 jioni na kufanikiwa kufikia juu ya kilele majira ya saa tano usiku.
“Tulianza matayarisho ya kuweka mwenge huku tukiwasiliana na wenzetu wa Dar es Salaam kwa njia ya redio.
“Ilipofika saa sita kamili usiku wa Desemba 9, tuliwasha mwenge tukio ambalo lilikwenda sambamba na kupandishwa kwa bendera ya uhuru wa Tanganyika katika Uwanja wa Taifa wa Uhuru jijini Dar es Salaam,” alisema Nyirenda
Kurejea Dar es Salaam
Baada ya kukamilisha shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kuweka alama hizo muhimu za uhuru, walirudi Dar es Salaam, ambako mji ulikuwa bado ‘ukichemka’ kwa shangwe na nderemo za uhuru kila kona.
“Tulipokelewa kwa furaha kubwa na Rais Nyerere ambaye alikuwa pamoja na mume wa Malikia wa Uingereza (Duke of Edinburgh) ambaye alikuwa amekuja nchini mahsusi kwa ajili ya sherehe za uhuru,” alisema Nyirenda katika mahojiano yaliyofanyika miezi michache kabla ya kifo chake.
Nyirenda alieleza kuwa, Mwalimu Nyerere alikuwa mtu ambaye alijitolea kuwa mtumishi wa dhati, na aliyefanya yote sio kwa ajili yake binafsi bali wananchi wake.
“Alitufundisha kuthamini wengine kwa kuweka neno “sisi” na sio “mimi”, yaani alitufundisha umoja, tuwe pamoja bila kutengana,” alieleza Nyirenda.
Kuugua na kifo chake
Kama kuna jambo lililowasikitisha wengi, ni kutelekezwa kwa muda kwa shujaa huyu baada ya kuanza kuugua ugonjwa wa saratani.
Askari huyu shujaa, alianza kupata msaada wa serikali pale tu vyombo vya habari vilipoanza kuandika na kutangaza habari za kuugua kwake. Ni serikali hiyo hiyo iliyogharamia mazishi yake baada ya kufariki dunia.
Alifikia cheo cha Brigeia Jenerali kabla ya kustaafu rasmi jeshi.
mtanganjia.blogspot.com
Home » Posts filed under MAKALA
WAJUE MAPRODUCER SABA WAKALI WALIOWAHI KUTOKEA KIPINDI HICHO | WACHEKI HAPA
P. FUNK MAJANI - BONGO RECORDS
Ipo wazi P.Funk Majani ni Legend katika mziki wa Tanzania,huyu jamaa ni mbaya sana katika kutengeneza beats kali, utakubaliana na mimi ukiskiliza nyimbo kama Mvua na jua ya Jay Mo,Anakuja ya Sister P, Nini mnataka ya Pig Black, Hayakuhusu ya Rah P, Kigetogeto ya Juma Nature na nyingine Chungu mzima.P Funk amewatoa wasanii wengi kama marehemu Ngwair(R.I.P),Juma Nature,Afande Sele, Sister P, Jay Mo, Profesa Jay na wengine chungu mzima.
MASTER JAY- MJ RECORD
Mmoja kati ya maproducer wanaojua haswa kufanya mixing kali ya musiki, anauwezo mkubwa sana wa kutambua na kuona kipaji cha mtu katika mziki.Aliweza kuibua vipaji vikubwa ambavyo vilifanya vizuri katika medani ya muziki wa Tanzania kama vile Lady Jay Dee ,Mike T Mnyalu bila kusahau Kundi la Kwanza Unit Ngoma ya Msafiri alitengeneza Master Jay na wengineo.
mtanganjia.blogspot.com
MIKA MWAMBA- FM STUDIO

Huyu ni moja ya kichwa kilichowakosesha usingizi watayarishaji wake kutokana na ubunifu wake wa hali ya juu, licha ya kufanya kazi nchini kwa muda mchache sana kabla hajarudi kwao ulaya lakini aliacha historia ya ngoma zake ambazo zinasikilizwa mpaka hii leo, mfano mzuri ni ngoma ya Balozi "wengi walikwepo", Salome ya Dully Sykes na bila kulisahau Kundi la Daz Nundaz.
HENRICO- SOUND CRAFTERS

Henrico ni mmoja ya watayarishaji wkongwe sana nchini hapa ambaye ameweza kuibua vpaji vingi haswa kwa wasanii wengi wa Temeke, Wasanii waliowahi kufanya kazi na Henrico ni kama Inspector Harun na kundi lake la Gangwe Mobb,Mabaga Fresh,Mack Malik Simba (R,I.P) ,Solo Thang na wengine wengi.
ROY WA G RECORD (R.I.P)- G RECORD

Enzi za uhai wake Roy alikuwa ni mmoja ya vichwa vikali kwenye utayarishaji wa midundo yenye ladha za upekee na utofauti mwingi, Roy aliweza kuinua vipaji kama vya kina Mr Blue,Enika -Baridi kama hii kama unaukumbuka ule mdundo utakuwa shahidi yangu.
SAID COMORIEN-METRO STUDIO

Comorien huyu alikuwa ni fundi wa vinanda, ukiwa ugonjwa wako ni vinanda basi tafuta ngoma alizotengeneza huyu mtu. Uwezo wake wa kukung'uta vinanda upo juu sana, sikiliza wimbo wa T.I.D wa nyota yangu usikie vile vinanda alivyoviingizia.Marehem Mez B (R.I.P) pia alishafanya kazi zake nyingi na Comorien bila kumsahau Noorah.
BONY LUV-MAWINGU STUDIO
Bony Luv ni mmoja ya maproducer wa zamani ambao ni multi-talented ,anauwezo mkubwa wa kutengeneza ngoma,kufanya mixing kali na ku dj pia.Amefanya kazi na wakongwe wengi wa zamani likiwemo kundi la Kwanza Unit waliorekodi santuri ya kwanza kabisa iliyoenda kwa jina la Kwanza Unit mwaka 1993.
Hawa ni baadhi tu ya watayarishaji waliowahi kuvuma sana enzi hizo, lakini wapo wengine wengi kama Amit Mento alitengeneza ngoma nyingi kali zikiwemo vituko uswahilini original na remix ya Suma G aliyomshirikisha Inspekta Haroun, pia ndiye alimyemtoa pia Mez B na ngoma ya kwanza iliitwa Fikiria, alitengeneza ngoma nyingi.za TID kama, siamini,nk pia ngoma ya Ray C uko wapi na Kuna nyimbo kama mambo safi ya Marehemu Complex,Big Dog Pose BDP majobless,na kumwambia. Pia kulikuwa na watayarishaji kama Akili The Brain, Kameta na wengineo
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
USISAHAU KUTEMBELEA mtanganjia.blogspot.com ILI USIPITWE NA HABARI ZA MAKALA KAMA HIZI ZINAZOKUJIA KILA SIKU.
e-mail - mtanganjia23@gmail.com
HUYU NDIYE CHE GUEVARA | JE UNAJUA KUWA ALISHWAHI KUISHI TANZANIA? | IJUE HISTORIA FUPI HAPA
Kazi : Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist)
Uraia : Argentina
Kuzaliwa : June 14 1928
Kufariki : October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera
Chanzo cha kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi
Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.
mtanganjia.blogspot.com
Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumng'oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.
Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata sifa ya kuwa mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema
wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?
Che ndani ya ukumbi wa UN mwaka 1964
miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha ,
Che Guevara akiwa Congo mwaka 1966
baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya UbepariĆ¢€¦aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores
mtanganjia.blogspot.com
KUKAMTWA NA KUUWAWAMwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,
Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
"Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa"
Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu Rena Barrientos kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale
Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
"Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili"
Aliacha wake wawili na watoto watano
mtanganjia.blogspot.com
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
USISAHAU KUTEMBELEA mtanganjia.blogspot.com ILI USIPITWE NA HABARI ZA MAKALA KAMA HIZI ZINAZOKUJIA KILA SIKU.
e-mail - mtanganjia23@gmail.com
10 TIPS FOR MINDFUL EATING — just in time for the holidays
Whether you want to avoid overeating and gaining those extra pounds, you need to control your blood sugar (for example, if you have diabetes), or you simply wish to consume only what your body requires, the holiday season can make that goal challenging.
But mindful eating might help you reach it.
Mindfulness refers to the practice of being aware and in the moment. All too often, our thoughts wander somewhere other than where we are in the moment. Perhaps we are preoccupied with what happened an hour ago, worried about what might happen tomorrow, or stressed over what we need to do next week. Mindfulness encourages us to notice these preoccupations, and then to gently bring ourselves back to the now.
Mindfulness can help you fully enjoy a meal and the experience of eating — with moderation and restraint. Some studies suggest that mindfulness-based practices help improve eating habits. For those who binge-eat or eat for comfort or out of stress, mindful eating may even aid with weight loss.
Here are 10 tips for more mindful eating. Not all of these tips may feel right for you — try a few and see how they work.
1. Reflect.
Before you begin eating, take a moment to reflect upon how you feel. Are you rushed? Stressed? Sad? Bored? Hungry? What are your wants, and what are your needs? Differentiate between the two. After you have taken this moment to reflect, then you can choose if you want to eat, what you want to eat, and how you want to eat.
2. Sit down.
Don’t eat on the go. Have a seat. You’re less likely to appreciate your food when you are multi-tasking. It’s also difficult to keep track of how much you are eating when you snack on the go.
3. Turn off the TV (and everything else with a screen).
Have you ever glanced down from your phone or tablet or computer, only to wonder where all the food went? These distractions make us less aware of what and how much we are eating.
4. Serve out your portions.
Resist eating straight from the bag or the box. Not only is it easier to overeat when you can’t see how much you’ve had, but it is also harder to fully appreciate your food when it is hidden from view.
5. Pick the smaller plate.
You might crave less if you see less. Smaller plates will help you with your portion control — an especially good strategy for those all-you-can-eat buffets.
6. Give gratitude.
Before you start to eat, pause and take a moment to acknowledge the labor that went into providing your meal — be it thanks to the farmers, the factory workers, the animals, mother Earth, the chefs, or even your companions at the table.
7. Chew 30 times.
Try to get 30 chews out of each bite. (30 is a rough guide, as it might be difficult to get even 10 chews out of a mouthful of oatmeal!) Take time to enjoy the flavors and textures in your mouth before you swallow. This may also help prevent overeating by giving your gut time to send messages to the brain to say you’re full.
8. Put down your utensil.
Often, we are already preparing the next morsel with our fork and knife while we are still on our previous bite. Try putting down your utensils after each bite, and don’t pick them back up until you have enjoyed and swallowed what you already have in your mouth.
9. Resign from the Clean Plate Club.
Many of us were brought up to finish everything on our plate and were not allowed to leave the table until we did. It’s okay to cancel your membership to the Clean Plate Club. Consider packing the leftovers to go, or just leaving the last few bites. Even though nobody likes to waste food, over stuffing yourself won’t help those in need. (This is also where Tip #5 comes in handy.)
10. Silence.
Try eating your meals in silence once in a while. When it’s quiet, it is natural for the mind to wander; acknowledge these thoughts, and then see if you can gently return to your experience of eating. Be conscious of the food’s consistency, flavor, tastes, and smells, and fully appreciate the moment. Of course, mealtime can be an important time for sharing the day when the whole household gathers, so having an entire meal in silence might be impractical or just feel awkward. But even spending the first five to 10 minutes in silence can be refreshing and set a grateful tone for the rest of the meal.
Mindfulness offers many benefits throughout the year, but can be especially helpful during the holidays, even beyond healthful eating. Purposefully focusing your attention on the present can help you embrace companionship, connectivity, and overall contentment and help make the season more meaningful for you.
