KALI YA MWAKA | WAUMINI KANISANI WASHEREHEKEA FILAMU HII

BOFYA HAPA UJISHINDIE ZAWADI YA GARI KILA SIKU=> CLICK AND WIN A CAR=> Click Here=>

Watoto walivalia mavazi ya Darth Vader kama ishara ya kusherehekea kwa kutolewa kwa filamu mpya ya Star wars katika kanisa moja jijini Berlin siku ya Jumapili

Waumini katika kanisa la Zion Church walianza ibada yao kwa kuonyesha mfululizo wa matukio kwa ufupi ya filamu hiyo ya Star Wars huku kasisi akiendeleza ibada hiyo kwa mafunzo kutoka kwa filamu hiyo.


Kasisi huyo akihutubia takriban waumini 500 alisema kuwa filamu hiyo ya Star Wars ina mafunzo ya kuhusu  kushinda ubaya kwa wema ambayo pia inapatikana katika Agano jipya la biblia ya kikristo.

Wakati huo huo baadhi ya vyombo vya habari vya kijamii vilikashifu kitendo hicho kanisani wakikosoa kwa kusemani kitendo cha dhambi na fedheha.

Lakini kasisi Eva-Maria Menard alisisitiza kuwa kushughulikia masuala ya kisasa na dini ni njia pia ya kuelimisha jamii zaidi.

FUNGUA HAPA KUSHINDA ZAWADI KEMKEM=>CLICK HERE TO WIN => Click Here=>

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top