Rnb staa Chris Brown ametoa maelezo ya kwanini halipishi wasanii ilikufanya nae collabo ikiwa ni tofauti na wasanii wengine nchini Marekani kama 2 Chainz ambaye huchaji mpaka dola laki moja kwa collabo moja.
Chris Brown anasema “sichaji pesa wasanii wenzangu sababu naandikia wasanii wengi na collabo nyingi nazo fanya na wasanii hao ni wasanii waliowahi kunasaidia kwenye nyimbo zangu so nikama narudisha fadhila tu, pesa nayopata kwenye collabo inatokana na mauzo ya wimbo kama single na mitandaoni, nakuwa nimeandika mashairi mwenyewe so napata asilimia yangu hapo “.
Sababu nyingine ya Chris Brown kutopenda kulipwa kwa collabo ni kuwa anapenda kujenga na kudumisha uhusiano mzuri na wasanii wenzake.
Chris Brown pia alisema “ kwa wasanii wanaochipukia huwa anatanguliza pesa yake anayotaka ya kufanya nao collabo sababu wimbo atakao fanya na msanii huyo utamtambulisha vizuri kwenye muziki na ni muhimu msanii kuthamini brand yako “.
Post a Comment