Mwanamuziki mahiri nchini Joh Makini ambaye anatamba na video yake na audio ya wimbo wake wa Do not Bother aliomshirikisha rapper mahiri kutoka Afrika Kusini A.K.A, amesema analazimika kutumia gharama kubwa katika video zake anazofanya ili azidi kujtangaza kwenye soka la muziki kimataifa.
Johmakini amesema kwa sasa ameishafika hatua za kimataifa hivyo ni vyema kwake kufanya video zenye hadhi ya kimataifa, kwa kulipa fedha kubwa katika video, huku akitaja gharama ambayo imetumika katika video ya Don't Bother na kueleza kuwa video hiyo imetumia kiasi cha shilingi 20.7, bila kuongezea manunuzi ya mavazi na vingine.
Johmakini amesema video hiyo imemfanya kuvunja rekodi ya video zote alizowahi kufanya na imemtengenezea wigo mpana kimataifa, pia ameongeza kuwa kuna kolabo na Davido inakuja ambayo inatarajiwa kutoka siku za hivi karibuni.
Post a Comment