HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imesema operesheni ya kuwakamata watu wote wanaoharibu na kuchafua mazingira wilayani humo, itaanza rasmi Desemba 9, mwaka huu ili kuhakikisha manispaa hiyo inabaki salama.
Tayari manispaa hiyo imeshaanza kutoa mafunzo kwa wakazi wa manispaa hiyo kabla ya kuanza utekelezaji wa operesheni hiyo baada ya Desemba 9.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu alisema wananchi wanatakiwa kupata mafunzo hayo baada ya muda huo kupita hakutakuwa na msamaha kwa mtu yoyote atakayeharibu na kuchafua mazingira.
“Mengi yako ndani ya uwezo wa mwanachi...hakuna kigumu cha kutushinda kwani afya ni ya kila mmoja wetu na ipo haja ya kutunza mazingira yetu,” Shaibu alisema.
Alisema wametoa muda huo wa mafunzo kwa wananchi ili kuwapa mwangaza wa kile kinachotaka kufanyika, ambapo muda utakapofika hapatakuwa na msamaha kwa watakaofanya makosa hayo.
Shaibu aliongeza kuwa kwa mujibu wa matangazo yanayoendelea kwa kutumia magari ya matangazo, ambayo ni mali ya manispaa hiyo ni moja ya njia ambazo wanatumia kwa kutoa elimu ya usafi wa mazingira.
Post a Comment