GOLI HILI LA KUSAWAZISHA LAUWA SHABIKI

BOFYA HAPA UJISHINDIE ZAWADI YA GARI KILA SIKU=> CLICK AND WIN A CAR=> Click Here=>



Habari za kusikitisha zimejiri huko nchini Hispania kufuatia matokeo yasiyotarajiwa ya sare ya 1-1 kati ya FC Barcelona vs Valencia.
 Katika mchezo huo Barca walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda ukizingatia mwenendo mbaya wa Valencia – Luis Suarez alifunga goli la Barca kufuatia assist ya Messi, lakini zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mchezo huo kuisha Valencia wakasawazisha wakati Santi Mina alipofumu shuti lilomshinda Claudio Bravo katika dakika ya 86.


 Gazeti/mtandao wa Marca unaripoti kwamba goli hilo lilimpa mshtuko shabiki wa Valencia aakati akishangilia  – shabiki huyo mwenye umri wa miaka 43 alipata mshtuko wa moyo, akapatiwa huduma ya kwanza lakini shabiki huyo akapoteza maisha yake hosptalini usiku wa jana.
Valencia wametoa taarifa rasmi wakionyeshwa kusikitishwa na kifo hicho na wamewapa pole mashabiki na familia ya shabiki aliyepoteza maisha. 
Mechi ya jana iliendelea kudumisha rekodi ya Valencia kutopoteza mechi katika uwanja wao wa nyumbani wa Mestalla baada ya kucheza michezo 7.
FUNGUA HAPA KUSHINDA ZAWADI KEMKEM=>CLICK HERE TO WIN => Click Here=>

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top