Lionel Messi amerudi tena kwa kasi ya aina yake kutoka majeruhi na kufunga goli murua huku Barcelona ikiwatungua River Plate ya Argentina kwa 3-0 na kuchukua ubingwa wa Club World Cup kwa mara ya tatu.
Messi alifunga goli lake mnamo dakika ya 36, kabla ya Muruguay Luis Suarez kuongeza mengine miwili mnamo dakika za 49′, 68′ katika mchezo uliopigwa kunako huko Yokohama.
Post a Comment