Will Smith amefanya show yake ya kwanza kwa baada ya miaka kadha nje ya muziki. Show hii ilikuwa kwenye jukwa la 16 la tuzo za Grammy za Latin America.
Mke wake Jada Pinkett-Smith na mtoto wao Trey walikuwepo kwenye show hio na kumuona Will Smith akifanya show pamoja na kundi la muziki kutoka colombia ‘Bomba Estéreo’ walipoimba wimbo wao wa ‘Fiesta’ remix. Show ilifanyika Las Vegas na hii ni show kubwa ya kwanza amefanya Will Smith baada ya ukimya wa miaka 10.
Smith anajibanga kurudi kwenye muziki na amesha rekodi nyimbo 30 na atafanya ziara na dj wake mkondwe DJ Jazzy Jeff.
Post a Comment