MOURINHO ATAKA ARSENAL IISHIE HATUA YA MAKUNDI UEFA,KISA HIKI HAPA

BOFYA HAPA UJISHINDIE ZAWADI YA GARI KILA SIKU=> CLICK AND WIN A CAR=> Click Here=>


LONDON,England

KOCHA wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa ni vema klabu ya Arsenal ikaishia katika hatua ya makundi katika michuano ya Uefa Champions League kuliko timu ya Olympiakos ya Uturuki ikaishia katika nafasi hiyo.Mourinho ambaye amerudi katika ubora wake wa kuongea hovyo mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi katika michezo miwili iliyopita,amesema kuwa anawaombea Olympiakos wapite na kufuzu katika hatua ya mtoano ya 16 bora kwa kuwa kocha wa timu hiyo Marco Silva ni rafiki yake wa siku nyingi.
Marco Silva
Amesema kuwa huwa anapendezwa na timu za Uingereza kufuzu katika hatua ya 16,lakini kwa hali jinsi ilivyo katika kundi F angependa timu ya swahiba wake huyo wa utotoni ikafuvu.
“Napenda timu za Uingereza zifuzu zote kwenda katika hatua ya 16,lakini kwa msimu huu ningependa timu ya Arsenal iishie katika hatua ya makundi ili kuipa nafasi Olympiakos kufuzu kwenda hatau inayofuata”
Pamoja na hayo huenda dua za kocha huyo wa zamani wa Real Madrid na Inter Milan ikawa ngumu kutekelezeka kwa kuwa mchezo unaokuja Arsenal watawakaribisha Olympiakos katika uwanja wao wa nyumbani huku wakitakiwa kuibuka na ushindi wa zaidi ya magoli 2-0 ili wajihakikishie kufuzu kwa kuwa na idadai ndogo ya magoli ya kufungwa.Hata hivyo huenda Chelsea nayo ikajikuta inashindwa kuendelea mbele kutoka katika kundi lake G kwa kuwa timu zote tatu za juu ikiwemo yenyewe zinanafsi ya kufuzu au kutokufuzu kwa kuwa mbili kwa maana ya Chelsea na Fc Porto zote zina alama 10 wakati anayeifuatia Dynamo Keiv ikiwa na alama 8
Arsenal inakamata nafasi ya tatu katika kundi F kwa kuwa na alama 6 na tofauti ya -1 ya goli la kufungwa wakati Olympiakos wenyewe wako katika nafasi ya pili wakiwa na tofauti ya -4 ya magoli ya kufungwa.
Bayern Munich inaongoza kundi hilo kwa kuwa na alama 12 ambazo zimewahakikishia kufuzu kwenda katika hatua inayofuata
FUNGUA HAPA KUSHINDA ZAWADI KEMKEM=>CLICK HERE TO WIN => Click Here=>

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top