NYON,Uswis.
KWA mara ya kwanza mshambuliaji mahiri wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar da Silva Santos amefanikiwa kuingia katika tatu bora ya wachezaji wanaowania tunzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon d’Or .Neymar ambaye amekuwa na msimu mzuri katika kikosi chake cha Barcelona na timu ya taifa Brazil ametajwa katika orodha hiyo sambamba na Lionel Messi na mshindi wa tunzo hiyo katika msimu uliopita Christiano Ronaldo.
Taarifa katika wavuti ya shirikisho la soka duniani FIFA ,imebainisha kuwa zoezi la kuwapata wanandinga hao limeendeshwa kwa kupigiwa kura na makocha na manahodha wa timu zote za taifa 207 ambao ni wanachama wa FIFA.Kuingia kwa kinda huyu wa kibrazili kunaweka historia ya kipekee katika taifa la Brazili ambalo kwa muda mrefu wachezaji wake hawakuwahi kuingia katika orodha ya tatu bora ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia(mara ya mwisho Ricardo Kaka 2007)
Aidha kuingia kwa mara ya kwanza kwa Neymar ni sawa na kutimia kwa kile kilichowahi kusemwa na Gwiji wa soka Duniani Edson Arantes do Nascimento ‘PELE’ kuwa mchezaji huyo ni dhahabu nyingine kutoka Brazili katika soka la Ulaya.Hata hivyo ,Neymar akiwa ndiyo kwanza ana misimu miwili anaungana na mchezaji mwenzake na nyota wa klabu ya Barcelona kumkabili Cristiano Ronaldo ambaye timu yake ya Real Madrid imekuwa haina matokeo mazuri katika mechi za hivi karibuni na kuufanya upinzani wa uwanjani katia ya Madrid na Barcelona kujitokeza tena katika tunzo za FIFA
Aidha hii itakuwa ni moja kati ya mafaniko makubwa kwa mwanasoka huyu machachari wa Brazili ambaye katika mwaka 2013 alikamata nafasi ya tano huku akiporomoka katika mwaka 2014 ambapo alikamata nafasi ya saba
Hii inamaana kuwa hii itakuwa ni mara ya tatu kwa wachezaji wa Barcelona kuchomoza wawili katika tunzo huku huku Madrid ikiwakiliswa na mchezaji mmoja,
MWAKA 2011
Lionel Messi-Barcelona
Cristiano Ronaldo-Real Madrid
Xavi Harnandes-Barcelona
MWAKA 2012
Lionel Mesi-Barcelona
Cristiano Ronaldo-Real Madrid
Andres Iniesta-Barcelona
MWAKA 2015
Neymar da silva Santos-Barcelona
Lionel Messi-Barcelona
Christiano Roanldo-Real MadridAidha hii imekuwa ni kama vita ya Madrid na Barcelona katika tunzo hii kwa kuwa kwa takribani miaka mitano nyuma wachezaji wa timu hizi mbili wamekuwa wakishirikishwa katika tunzo hii katika hatua ya tatu bora.
REKODI INAVYOMBEBA MESSI.
Pamoja na kutokuwa katika hali yake ya kawaida kutokana na kutoka katika majeraha,Lionel Messi anaweza kufanikiwa kunyakua Tunzo hii kwa mafaniko mbalimbali ambayo ameipa timu yake.Kunyakua taji la ligi ya mabinga Ulaya mwezi mei mwaka huu,pamoja na kubeba taji la ligi kuu Hispania na jitihada zake dimbani huenda zikawa sababu pekee za mshambulijai huyu kutunukiwa tunzo hii ambayo kama itakuwa hivyo hii itakuwa ni tunzo yake ya tano ya mchezaji bora duniani.Lakini kumbukumbu zinaonyesha kuwa kila orodha hii inapotangazwa na kuhusisha wachzaji zaidi ya mmoja wa Barcelona katika tatu bora,Lionel Messi amekuwa akimbwaga vibaya mpinzani wake Ronaldo.
NAFASI YA NEYMAR.
Pamoja na machacahri yake aliyoyaonyesha hivi karibuni ya kufunga magoli katika kila mechi bado huenda asifikiriwe kupewa tunzo hii kutokana na kutokuwa na rekodi nzuri za nyuma haswa katika soka la Ulaya.
Hii inahusishwa kutokana na upinzani wa wachezaji wenzake ambao wote wanahistoria ya kutwaa tunzo hii zaidi ya mara mbili,wakati yeye hajawahi kutwaa hata mara moja.
Pamoja na hayo bado anaweza kushika nafasi ya pili kutokana na mchango wake katika timu yake ya taifa na klabu ya Barcelona.
RONALDO AJIPANGE MWAKANI.
Huenda hili likamkwaza sana Ronaldo ikizingatiwa kuwa anataka kumpiku Messi ambaye anatunzo nne yeye akiwa na tatu,hivyo dua zake zote anaelekeza kwa wapigaji kura ili wamchague aweze kutwaa tunzo hiyo mara ya nne kama Messi.Lakini ukweli utabaki kuwa katika kipindi cha hivi karibuni Ronaldo ameshindwa kuisaidia klabu yake katika baadhi ya mashindano huku kipigo cha juzi katika mchezo wa ligi dhidi ya Barcelona kikitajwa kuwa kinaweza kumyima nafasi hii,japo naye anaweza kutwaa kama wapiga kura wataangalia kigezo cha mafaniko binafsi nnje ya klabu kwani hivi karibuni alitwaa tunzo ya mchezaji bora wa Ulaya,kumbuka kuwa Ronaldo ndiyo mtetezi wa tunzo ya sasa ya mchezaji bora wa Dunia
HISTORIA YA RONALDO NA MESSI KATIKA BALLON d’Or
Messi am,eanza kushirikishwa katika tunzo hizi mwaka 2008 ambapo hii itakuwa ni mara yake ya 8 kushiriki katika tunzo hizi,ambapo katika mara zote nane ametwaa mara nne na kuambulia patupu mara nne
Ronaldo ameshiriki katika tunzo hizi mara 9 toka mwaka 2007 ambapo katika kipindi chote hiko ametwaa tunzo hii mara 3 na kuikosa mara 6 ikiwemo mara nne kwa macho yake akiona inakabidhiwa kwa hasimu wake Messi
SWALI;-
Je wabrazili wanaweza kusherekea tunzo hii kwa mara nyingine tena mara baada ya kupelekewa na Ricardo Kaka mwaka 2007?

Post a Comment