SABABU ZA CAF KUKATAA OMBI LA YANGA KUCHEZA TAREHE 29, KUELEKEA MECHI NA TP MAZEMBE.

Baada ya CAF kukataa kuusogeza mbele mchezo wa Yanga sc dhidi ya TP Mazembe ambao Yanga walipendekeza uchezwe tarehe 29 mwezi huu lakini CAF wamesimama kwenye maamuzi yao na mchezo kubakia kama ilivyopangwa.
NA je baada ya mmiliki wa TP Mazembe kupata kesi na kuhukumiwa kwenda miaka mitatu jela je itaiathiri klabu hiyo.Bofya hapa chini kupata uhondo wa wachambuzi mahiri Tanzania.


Official VIDEO | BARO MASTER - I SAW | Dir by Ubwa

https://www.youtube.com/watch?v=WxKyzgYfPBE


http://www.youtubeinmp4.com/redirect.php?video=WxKyzgYfPBE&r=v3ArBAS5KSlZvesGrje8ta6vFcdtTJqQPaUZ0npQnW4%3D

Serikali Yakanusha Madai Kuwa Haina Mpango wa Kuwapanga Vijana Waliohitimu Kidato cha Nne kwenda kidato cha Tano


Serikali imekanusha madai ya  kuwepo kwa taarifa ya kuwa haina mpango wa kuwapanga vijana waliohitimu kidato cha nne kwenda kidato cha tano kwa sababu mbalimbali.

Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa taarifa hizo ni za uvumi na serikali kwa sasa ipo katika mchakato wa upangaji wa majina hayo na wakati wowote mwisho mwa mwezi majina yatakuwa yametolewa.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema moja ya sababu za kuchelewa kwa matokeo hayo ni pamoja na wizara kubadili mfumo wa GPA, kwenda Division hivyo mchakato huo ndio unafanywa na serikali ili wanafunzi wote wapate madaraja yao na waweze kupangiwa shule.

Mhe. Majaliwa amesema suala la upangaji halikuwa kwa kidato cha tano peke yake bali pia wale wanaokwenda vyuo mbalimbali na kusema kuwa baada ya kukamilika watatoa majibu yao wiki mbili kabla ili wazazi waweze kujiandaa kuwapeleka watoto mashuleni.

Magufuli: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Pumzika Kwa Amani.......Wewe upo Salama, Usisikilize kelele za Nje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kwamba serikali itawalinda wastaafu nchini wakiongozwa na viongozi wakuu wa umma ili wawe na heshma yao ndani ya jamii.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa tume ya taifa ya uchaguzi.

''Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wewe pumzika kwa raha zako , upo salama watachonga wee lakini mimi kama Rais wa awamu ya tano nipo tayari kuwalinda watumishi wote wastaafu kwa kuthamini mchango wao ndani ya taifa hili''

Aidha Rais Magufuli amesisitiza kwamba uchaguzi nchini umemalizika hivyo vyama vyote vya siasa viongeze nguvu baada ya miaka mitano ili apimwe na wananchi waliomchagua kama ametekeleza ahadi zake.

''Niwaombe wanasiasa wenzangu uchaguzi umekwisha, kama ni wabunge jielekezeni bungeni, kama ni madiwani jielekezeni kwenye maeneo yenu, sitakubali mtu yeyote anikwamishe katika kutimiza ahadi zangu kwa wananchi'' Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu tume ya uchaguzi kukabiliwa na changamoto lukuki Rais Dkt. Magufuli amesema fedha za tume hiyo ilizobakiza kiasi cha shilingi bilioni 12 na kuzirudisha serikalini, serikali imeruhusu fedha hizo zitumike kujenga jengo la tume hiyo ili kuondokana na gharama za kupangisha jengo wanalotumia kwa sasa.

Aidha akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva amesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa huru na wa haki na hata waangalizi wa nje wengi wamepongeza uchaguzi huo.

VIONGOZI WA CUF WAPONDWA KWA KUKOSA UZALENDO.


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekishiutumu Chama cha Wananchi (Cuf) pamoja na viongozi wao kwa kukosa uzalendo kutokana na kauli zao za kuunga mkono wahisani kuisitishia misaada Tanzania.

Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa kuteuliwa kutoka katika chama cha Ada-Tadea, Juma Ali Khatib ambaye aligombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa marudio, alipokuwa akichangia hotuba ya Rais wa Zanzibar kwenye baraza hilo mjini hapa.

Alisema, viongozi wa Cuf wameonesha udhaifu mkubwa wa kukosa uzalendo kwa kitendo chao cha kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa misaada kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema, Zanzibar ni nchi yenye kufuata katiba yake kwa hiyo ilikuwa na mamlaka kamili kupitia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kuitisha uchaguzi wa marudio baada ya kuufuta wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Nimesikitishwa na kauli za viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kuhusu uamuzi wa kususia misaada kwa Tanzania. Viongozi hao wameonesha udhaifu na kukosa uzalendo,”alisema Khatib.

Alisema chama chake kiliamua kuingia katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kwa sababu umeitishwa na chombo halali kwa mujibu wa katiba, chenye majukumu ya kusimamia uchaguzi kikiwa hakiingiliwi na mtu yeyote.

Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini , Machano Othman Said, alisema kitendo cha viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa kutoa misaada kwa Tanzania hakikubaliki hata kidogo kikionesha udhaifu mkubwa wa viongozi hao katika uzalendo wa nchi.

SAKATA LA DIAMOND KUTOBOA PUA HILI HAPA


Kwa saa kadhaa zimeenea taarifa za mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kuonekana katoboa pua, hii habari imepewa nguvu kutokana na picha aliyoipost Diamond mwenyewe kwenye Instagram akionekana katoboa pua.
Ukweli ukoje? …ukweli ni kwamba Diamond hajatoboa pua kama wengi walivyodhani ambapo Meneja wake aitwae Sallam aliwajibu hivi mashabiki walioanza kuuliza >>> ‘Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo’
SK
Maneno ya Meneja Sallam yanamaanisha kwamba sio kweli Diamond katoboa pua, ni mchezo tu na baada ya hiyo picha ya kutoboa pua Diamond aliweka picha nyingine inayoonekana hapa chini akiwa fresh kabisa watu wasiendelee kupanic.
Diamond 2

PICHA MBALIMBALI ZA RAIS MAGUFULI AKIWA NA RAIS KAGAME NCHINI RWANDA










Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top