MKUU WA MKOA AAGIZA OMBAOMBA ‘WASAFISHWE’ KATIKA MAENEO YAO SIKU YA USAFI 9/12

BOFYA HAPA UJISHINDIE ZAWADI YA GARI KILA SIKU=> CLICK AND WIN A CAR=> Click Here=>



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchi.
Sadiki amesema utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu.
“Siwezi kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo,” amesema.
Amesema viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi, wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.
Aidha, ameiiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaondoa wapigadebe katika vituo vya daladala kwani wamekuwa kero kwa abiria.
FUNGUA HAPA KUSHINDA ZAWADI KEMKEM=>CLICK HERE TO WIN => Click Here=>

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top