IVO MAPUNDA ASAINI MKATABA NA AZAM FC

BOFYA HAPA UJISHINDIE ZAWADI YA GARI KILA SIKU=> CLICK AND WIN A CAR=> Click Here=>

Kikosi cha timu ya Azam FC kimempa mkataba wa muda mfupi golikipa wa zamani wa vilabu vyaTanzania Prisons, Yanga na  Simba vya Tanzania Ivo Mapunda baada ya kuridhishwa na uwezo wa mlinda mlango huyo aliyekuwa akifanya mazoezi ya kujiweka fiti na kikosi cha Azam baada ya kutemwa na klabu ya Simba kabla ya kuanza kwa msimu huu.
Mtendaji mkuu wa Azam FC Saad Kawemba amethibitisha taarifa hiyo ya kusajiliwa kwa Ivo Mapunda kujiunga na Azam kwa mkataba wa muda mfupi.
“Tumempa mkataba wa muda mfupi kwasababu yeye mwenyewe anasafari ya kutoka nje ya nchi ambayo sisi pia tutaendelea kumsaidia, mwezi June atakuwa anatoka anakwenda nje ya nchi. Tukianza ligi baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa, Ivo atakuwa ni golikipa wetu na hakutakuwa na pingamizi katika hilo”, amesema mtendaji mkuu wa klabu ya Azam FC Kawemba.
Mapunda amekuwa akifanya mazoezi na klabu ya Azam kwa miezi mitatu sasa tangu alivyoachwa na klabu ya Simba kwa madai kwamba alikuwa akikwepa kusaini mkataba mpya aliokuwa akipewa na uongozi wa timu hiyo kitu ambacho Mapunda alisema si kweli.
Ivo Mapunda amewahi kuvitumikia vilabu kadhaa vya nje ya nchi ikiwemo St George ya Ethiopia pamoja na klabu ya Gor Mahia ya Kenya kabla ya kurejea nchini na kujiunga na ‘Wekundu wa Msimbazi’, Simba.
FUNGUA HAPA KUSHINDA ZAWADI KEMKEM=>CLICK HERE TO WIN => Click Here=>

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright MTANGANJIA Published.. Blogger Templates
Back To Top