Msanii anaeiwakilisha vyema miondoko ya R$B kutoka mkoani morogoro maarufu kama BELLE 9 amepata shavu la kuwa balozi wa mtandao wa owbaz, mtandao ambao unahuska na masuala ya ajira.
Akizungumzia mtandao huo Belle 9 amesema kuwa utasaidia kukuza soko la ajira kwani vijana wengi wamekuwa wakimaliza masomo bila kupata ajira, hivyo kupitia taaluma zao mbalimbali wanaweza pata ajira na kuboresha maisha yao
Kuhusu suala la mkataba wake na owbaz Belle 9 amesema mkataba wake ni wa muda mrefu, hivyo mashabiki wake wake na watanzania watarajie, uwakilishi mwema katika kampuni hiyo kwa mustakabali wa soko la ajira nchini.
Post a Comment